Siasa sasa zapelekwa WhatsApp uchaguzi wa 2027 ukikaribia
KATIKA siasa za Kenya za sasa, mapambano makali hayafanyiki tena kwenye mikutano ya hadhara, Bunge au runinga pekee. Makundi yaliyoundwa awali kwa ajili ya kuratibu shughuli na kuhamasisha wafuasi sasa yamegeuka kuwa uwanja wa kupimana nguvu, kujenga au kuvunja ushirikiano na kuonyesha uaminifu wa kisiasa.
