Wito wa uwekezaji katika Kiswahili ili kisibaki nyuma kidijitali
Waliohudhuria walijumuisha wasomi kutoka vyuo vikuu vya Afrika Mashariki na maafisa kutoka taasisi za lugha, wawakilishi wa mashirika ya serikali, mashirika ya kitamaduni, pamoja na wasomi kutoka vyuo vikuu vya Marekani. Mwaka 2021, shirika la UNESCO lilitangaza Julai 7 kuwa Siku ya Kiswahili Duniani, ikiwa ni mara ya kwanza kwa lugha ya Kiafrika kupewa hadhi hiyo ya kimataifa.
