TAHARIRI: El Nino sasa imekaribia, tukae ange
KWA muda wa miezi kadhaa, wataalamu wa hali ya anga wamekuwa wakiutahadharisha ulimwengu kuhusu ujio wa mvua ya El Nino. Kulingana na ripoti za kitaalamu, kipindi cha kuanza kwa mvua hiyo inayotarajiwa kuzua madhara tele kimewadia.
