Ruto akabiliwa na ugumu wa kuridhisha wapigakura wa Nyanza
RAIS William Ruto anakabiliwa na kitendawili cha kuvutia uungwaji wa wapigakura wa Luo Nyanza, ikisalia miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu 2027. Kilichosawiriwa kama ishara ya umoja kabla ya ziara ya siku nne ya Rais Ruto eneo la Nyanza, kiligeuka upesi pale ushindani ulipochipuka pamoja na orodha ya matakwa kutoka kwa uongozi wa ODM.
