Takwimu za CBK zaonyesha Wakenya wanakopa sana kumudu mahitaji ya kila siku
HALI ngumu ya maisha imesukuma mamilioni ya Wakenya kutafuta mikopo ya kidijitali ili kukidhi mahitaji ya kila siku, huku zaidi ya akaunti milioni nane zikikopa zaidi ya Sh150 bilioni. Takwimu za Benki Kuu ya Kenya (CBK) zinaonyesha kuwa mikopo hiyo mingi haitumiki kuanzisha biashara au kuwekeza, bali kugharamia matumizi na mahitaji ya kimsingi ya maisha.
