Amerika yamezea mate madini ya Kenya bila kuficha
Amerika imeongeza hamu yake katika madini muhimu ya Kenya wakati ambapo serikali ya Rais William Ruto inataka kuendeleza uwezo wa kuchakata madini ndani ya nchi badala ya kuyauza nje yakiwa ghafi. Suala hilo lilijitokeza kwa uzito wakati wa mkutano kati ya Rais Ruto na Waziri wa Masuala ya Kigeni wa Amerika, Marco Rubio, Septemba 21, pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA) jijini New York.
