Serikali yataja fursa Geita, yahimiza wananchi kuzichangamkia
Serikali imetaja sekta ya madini, kilimo, ufugaji wa samaki, ujenzi na huduma za chakula kuwa miongoni mwa maeneo yenye fursa za kiuchumi kwa wananchi mkoani Geita, huku ikiwataka kuchangamkia fursa hizo ili kuongeza kipato na kujenga uchumi wa kaya.
