Jinsi ya kutambua walaghai wa mapenzi wanakunyemelea mtandaoni
Kadri watu wengi wanavyotumia mitandao na apu za kutafuta wachumba, ndivyo matapeli wa kimapenzi wanavyozidi kuwanasa waathiriwa wao. Utafiti wa TransUnion unaonyesha kuwa karibu Wakenya watatu kati ya kumi wanaotumia apu za uchumba mtandaoni wamewahi kukumbana na jaribio la ulaghai.
