Pombe haramu yaua watatu Kitengela, wawili mahututi
Huzuni imetanda katika kijiji cha Noonkpoir, Kitengela, Kaunti ya Kajiado, baada ya watu watatu kufariki dunia na wengine wawili kulazwa hospitali wakiwa mahututi kutokana na kile kinachoshukiwa kuwa pombe haramu. Mnamo Ijumaa asubuhi, Christine na jamaa zake waliomboleza kifo cha mumewe, James Maina Nguru, aliyefariki Jumatatu usiku baada ya kunywa pombe hiyo.
