Ushindi kwa serikali Mahakama ya Rufaa ikiunga ushuru wa nyumba
Mpango wa Rais William Ruto wa nyumba za bei nafuu umepata nguvu kubwa baada ya Mahakama ya Rufaa kuidhinisha sheria ya makazi nafuu na ushuru wa nyumba, huku ikitupilia mbali kesi 42 zilizopinga sheria hiyo. Katika uamuzi wake, jopo la majaji watano lilisema Sheria ya Makazi Nafuu ilitungwa ili kutekeleza haki ya kila Mkenya kupata makazi bora na ya kutosha kama ilivyo katika Katiba.
