Uchumba wa Rigathi, Sifuna kisiasa utautikisa upinzani
Huku baadhi ya wadau wakichukulia ushirikiano huo kama silaha ya kumenyana na Rais William Ruto, wengine wanahisi unaweza kuwa chanzo cha migawanyiko mipya ndani ya upinzani. Aliyekuwa Seneta wa kuteuliwa Gloria Orwoba ni mmoja wa waliozua mjadala huo baada ya kusema Wakenya wasipuuzilie mbali uwezekano wa Gachagua na Sifuna kujitokeza pamoja kwenye tiketi ya urais mwaka 2027.
