Kauli tata ya Kalonzo kuhusu ‘uwezekano wa kufanya handisheki na Ruto’ yazua gumzo
KIONGOZI wa Wiper Kalonzo Musyoka amezua mjadala kuhusu msimamo wake wa kisiasa baada ya kuonyesha dalili ya kuwa atashiriki handisheki na Rais William Ruto upinzani ukishindwa uchaguzi wa 2027. Bw Musyoka amesisitiza kuwa siasa za ushindani kati ya Rais Ruto na vinara wa upinzani inastahili kuzingatia masuala yanayohusisha maslahi ya nchi badala ya uhasama wa kisiasa.
