Stendi ya Segerea yaanza kukarabatiwa, madereva wasema…
Madereva, wafanyabiashara na wadau wa usafirishaji katika Stendi ya Daladala ya Tabata Segerea jijini Dar es Salaam wameipongeza Serikali kwa kuanza ukarabati wa miundombinu ya kituo hicho, wakisema hatua hiyo itasaidia kuondoa kero ya mashimo iliyodumu kwa zaidi ya miaka miwili.
