IEBC kusajili wapigakura wapya kutoka mataifa 26 Ughaibuni
TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imepanua usajili wa Wakenya wanaoishi ughaibuni kutoka nchi 12 hadi 26, hatua inayolenga kuwapa Wakenya wengi zaidi nafasi ya kushiriki uchaguzi mkuu wa Agosti 2027. Wakati huo huo, tume hiyo imekanusha madai kwamba inasajili raia wa nchi jirani kuwa wapigakura nchini Kenya.
